20th February, 2018
Waziri mpya wa michezo Rashid Echesa Mohamed ametwaa hatamu za uongozi wa wizara hiyo huku akiwaonya wafanyikazi wa wizara na wadau wa michezo dhidi ya ukiritimba. Aidha amedokeza kwamba atatilia maanani miundo misingi huku akiwamba wadau kumpa muda.