15th February, 2018
Mkenya pekee katika mashindano ya olimpiki ya nyakati za baridi Sabrina Wanjiku Simader alishiriki mashindano yake ya kwanza hapo jana katika kitengo cha giant slalom. Sabrina aliye na umri wa miaka 19 aliorodheshwa kwenye nafasi ya 59 akiandikisha muda wa dakika 1 sekunde 27. Watelezaji 67 pekee kati ya 81 walioshiriki walifanikiwa kumaliza. Sabrina atajitosa thelujini tena hapo kesho katika fainali kabla ya kushiriki tena siku ya jumamosi katika kitengo cha super giant.