×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Mali ya thamani yateketea katika mkasa wa moto Kenya Pipeline-Kisumu

14th February, 2018

Mali ya thamani ya mamilioni ya pesa imeteketea jijini Kisumu baada ya moto kuzuka kwenye vibanda viliyo mkabala wa kampuni ya mabomba ya kusambaza mafuta ya Kenya Pipeline.  Moto huo ambao umewaacha watu wawili wakiuguza majeraha mabaya unadaiwa kusababishwa na gari lililokuwa likivuja mafuta aina ya petroli. Kwa mujibu wa wakazi, gari hilo liligonga matuta ya barabara kabla ya kulipuka. Wakazi hata hivyo wamelaumu wazima moto kutoka kampuni ya Kenya pipeline na wenzao kutoka serikali ya kaunti kwa kuchelewa kufika na kusababisha moto huo kusambaa kwa kasi. Kamanda wa polisi katika kaunti ya Kisumu John Kamau, amesema polisi wameanzisha uchunguzi kufuatia mkasa huo.

.
RELATED VIDEOS