31st January, 2018
Kigogo wa zamani wa AFC Leopards Joe Kadenge amewahimiza washikadau wa kandanda wazindue mifumo ambayo itawasaidia wachezaji wa zamani. Kadenge, atapata fursa ya kutazama mechi ya ligi kuu nchini Uingereza kati ya Manchester United na Huddersfield uwanjani Old Trafford siku ya jumamosi kupitia udhamini wa kampuni ya Black Arrow.