.
29th January, 2018
Chama cha wahariri nchini kinaelezea wasiwasi kwa kile kinasema ni njama ya serikali ya Jubilee kukandamiza Uhuru wa vyombo vya habari nchini. Kwenye taarifa iliyotolewa baada ya mkutano uliofanyika hapa Nairobi, wahariri hao chini ya uenyekiti wa Linus Kaikai wamekosoa mkutano unaoripotiwa kuandaliwa katika ikulu ya nairobi ambako baadhi ya wahariri walihudhuria ikulu. Kwenye mkutano huo, Rais Uhuru anaripotiwa kutisha kufunga baadhi ya vyombo vya habari na kubatilisha leseni iwapo watapeperusha hafla ya uapisho wa Raila Odinga na Kalonzo Musyoka