Muungano wa upinzani NASA wasema kuwa mipango ya kumuapisha Raila Odinga kama rais imo mbioni

Dira ya Wiki | Friday 26 Jan 2018 7:49 pm

Muungano wa upinzani, NASA, umetoa matokeo yake kuhusu uchaguzi wa tarehe nane mwaka uliopita na kudai kwamba Raila Odinga alishinda kinyangányiro hicho lakini akapokonywa ushindi. Kulingana na matokeo hayo, Raila Odinga alipata kura milioni 8.1, huku Uhuru Kenyatta akipata kura milioni 7.9. Aidha, kaimu mwenyekiti wa tume ya IEBC Connie Maina amepuzilia mbali matokeo hayo na kuyataja kama hekaya za NASA.