Jaji mkuu David Maraga atoa wito kwa wabunge wa kamati ya sheria

Dira ya Wiki | Friday 26 Jan 2018 7:43 pm

Jaji mkuu David Maraga ametoa wito kwa kamati ya sheria bungeni kupitisha mswada wa kutengwa fedha zaidi kwa idara ya mahakama ili kuboresha utendakazi. Maraga ambaye alifungua rasmi warsha ya uhamasiho kwa wabunge wa kamati hiyo jijini Mombasa alitangaza kuwa tayari idara ya mahakama inanuia kutumia teknolojia katika shuguli zake kama vile usajili wa kesi na kuhifadhi stakabadhi za kesi. Maraga aidha alikemea ufisadi ambao alisema ni hatari kwa usimamizi wa haki.