.
23rd January, 2018
Wanawake hapa Nairobi wamefanya maandamano ya amani kukashifu vitendo vilivyoripotiwa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta. Majibizano makali yalishuhudiwa baina ya kikundi hicho kilichoanza maandamano yake katika bustani ya Uhuru na wafanyikazi wa hospitali hiyo. Maandamano hayo yanalaani tuhuma za ubakaji wa wanawake waliojifungua hospitalini humo.