23rd January, 2018
Wanawake hapa Nairobi wamefanya maandamano ya amani kukashifu vitendo vilivyoiripotiwa katika hospitali ya kitaifa ya kenyatta. Maandamano hayo yalianzia bustani ya Uhuru kuelekea ofisi za wizara ya Afya na kisha hospitalini Kenyatta, kulaani vikali tuhuma za ubakaji wa wanawake waliojifungua.