×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Wazazi wawili watia nguvuni Nakuru baada ya kuwazuilia wanao wanne kwa sababu za kidini

19th January, 2018

Wazazi wawili wametiwa nguvuni katika kaunti ya Nakuru baada ya madai kuibuka kwamba wamewazuia watoto wao wanne kupata elimu kwa sababu za kidini. Solomon Orwa na mkewe Eunice Akoth walitiwa nguvuni mapema leo baada ya wazee wa kijiji kuwajulisha maafisa wa polisi. Kulingana na chifu wa eneo hilo watoto hao wamefungiwa ndani ya nyumba kwa zaidi ya miezi sita. Inadaiwa kuwa watoto hao waliachishwa shule julai mwaka uliopita baada ya madai kwamba imani yao haiwaruhusu kwenda shuleni. Wazazi hao wamekiri kosa hilo wakijitetea kuwa suala la shule halimo kwenye bibilia kwa hivyo itakuwa dhambi kulizingatia. Wazazi hao wakidai kwamba wana haki ya kikatiba ya kufuata imani wanayotaka. Kulingana na mmoja wa watoto wao wa umri wa miaka 13 anayefaa kuwa darasa la nane mwaka huu, wazazi wake walimsihi kuacha shule baada ya kudai kwamba masomo yangeiharibu imani yake. 

.
RELATED VIDEOS