17th January, 2018
Mtazamaji je wafamu kuwa pombe ya busaa ni dawa ya maradhi fulani fulani kwa mifugo? Haya yanashuhudiwa huko Nakuru amabpo wafugaji wafugaji wameamua kutumia pombe aina ya busaa kutibu maradhi ya miguu na midomo kwa mifugo wao.Hata hivyo vigngozi wa maeneo hayo sasa wana hofu kwamba kusambaa kwa busaa na matumizi yake kunaweza kukithi mipaka na kukosa kudhibitiwa. Wafugaji hao wanalilia hasara kutokana na ugonjwa huo hatari kwa ng’ombe wao na wanailaumu serikali ya kaunti ya nakuru kwa kukosa kuchukua hatua za dharura ili kukabiliana na ugonjwa huo wanaodai utawaacha masikini hohe hahe.