×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Ajuza ateketezwa mjini Kisii kwa madai ya ushirikina

17th January, 2018

Tunaanza huko Kisii  eneo bunge la bonchari ambapo ajuza mmoja wa umri wa miaka sabini na mmoja ameshambuliwa na kuuawa kufuatia kifo cha ghafla cha mjukuwe mwenye umri wa miaka kumi na miwili maxwell miruka. Wenyeji walimshuku bibi  huyo kuwa amemroga mjukuwe, na ndipo wakabomoa nyumba yake iliyoezekwa kwa majani na kumteketeza moto hadi kufa. Ajuza huyo inadaiwa aliwahi kuahidi kutoa adhabu kali kwa watu waliohusika kwenye wizi wa matunda yake na hivyo basi mjukuu wake alipoaga baada ya kuugua maumivu ya kifua usiku mmoja  wenyeji wakachukua sheria mikononi kwa kutumia imani za ushirikina.  Polisi walichukua mabaki ya marehemu  mama biyaki kemunto aliyeishi katika kijiji cha  bokoma kata ya riana, na kuupeleka katika hifadhi ya maiti ya  hospitali ya  rufaa ya kisii. 

 

.
RELATED VIDEOS