Timu ya Kenya yabombea katika mashindano ya tenisi

Sports | Friday 12 Jan 2018 8:09 pm

Timu ya Kenya ilibobea katika mashindano yanayoendelea ya tenisi ya kanda ya Afrika mashariki. Kwenye kitengo cha wavulana wenye umri wa miaka 14, mchezaji wa Kenya Brandon Sagala alimbwaga Hassan Rouchedi kutoka Comoros kwa seti 6?1, 6?0 katika mechi ya kwanza, huku mkenya Kael Shah akishinda mechi ya pili 2?0 kwa kusajili 6?0, 6?1 dhidi ya mchezaji antoissi mohammed kutoka comoros. kwenye mechi tofauti, Sagala na Shah waliwabwaga Mohamed na Yassini kutoka Comoros seti mbili bila jibu. Katika kitengo cha akina dada wenye umri usiozidi miaka16, Mkenya Angela Okutoyi alimlaza mshindani wake kutoka Uganda, Shanitah Namagembe, kwa huku mkenya Sneha Kotecha akiibuka mshindi kwenye mechi ya pili.