Kikosi cha raga cha Nakuru RFC wafanya mabadiliko kwa kikosi mbele ya mchuano dhidi ya Black Blad

Sports | Friday 12 Jan 2018 8:04 pm

Kikosi cha raga cha Nakuru RFC kimefanya mabadiliko ya wachezaji watatu kwenye kikosi chao kilicho lazwa na KCB, huku wakijiandaa kwa mechi yao muhimu dhidi ya Blak Blad siku ya jumamosi. Wachezaji Sammy Warui, Philip Kwame na Cassius Omollo wamekosa kujumuishwa katika kikosi chao huku emmanuel mboya, Steve Wamae na Gramwel Bunyasi wakichukua nafasi zao.  Bada ya kulazwa 48?20 dhidi ya Quins na 70?16 dhidi ya KCB, wapinzani wa Nakuru ambao ni Blad watakuwa wakijaribu kutafuta ushindi kwenye mechi hio. Hata hivyo nakuru wamekosa kushinda mechi tatu zilizo pita hii ikiwa ni baada ya kulaza Kisii RFC na ari yao ni kuwa na matokeo mema.