Mohammed Abdi atapoteza kiti cha gavana cha Wajir baada ya koti kufutilia mbali ushindi

Dira ya Wiki | Friday 12 Jan 2018 7:21 pm

Gavana wa kaunti ya Wajir Mohammed Abdi atakuwa wa kwanza kupoteza kiti chake baada ya mahakama kuu ya Milimani mjini Nairobi kufutilia mbali ushindi wake kwa msingi kwamba hakuwa na cheti halali cha shahada.