8th January, 2018
Viongozi kutoka kitui mashariki wamesisitiza kuwa watahakikisha kuwa wanawaondoa wafugaji wanaotoka kasikazini mwa kenya wanaoishi katika mpaka wa Kitui. Haya yanajiri huku kukiwa na madai kuwa wafugaji wanaotoka wajiri na mandera walizivamia zaidi ya familia kumi na kuwajeruhi watu kutokana na mzozo wa malisho ya mifugo. Akizungumza katika eneo la malalani mbunge wa eneo hilo nimrod mbai amedai kuwa wafugaji hao ni tishio kubwa kwa wenyeji na itakuwa bora ikiwa wangeondoka mara moja. .naibu kamishna wa kaunti anayesimamia eneo la Mutito Benjamin Nzioka pia alitoa ushauri huo.