10th November, 2016
Wabunge wawili mjini Nakuru Samuel Arama na David Gikaria wameongoza wananchi kuvamia kampuni moja katika mtaa wa Shabab na kumkamata polisi bandia, mlinzi aliyekuwa ameajiriwa na kiwanda hicho na kuruhusiwa kumiliki bunduki ili kutoa ulinzi kwa wafanyikazi ilhali yeye si afisa wa polisi. Maafisa wa polisi nao wakilazimika kuwarushia waandamanaji hao vitoza machozi na kuwatawanya, huku OCPD wa Nakuru Joshua Omukata akikiri kutomfahamu polisi huyo bwege na kuahidi kufanya uchunguzi zaidi.