5th October, 2016
Timu ya taifa ya kandanda Harambee Stars iliwaduwaza Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo bao moja bila jibu ugenini katika mechi ya kirafiki iliyochezwa hapo jana usiku mjini Kinshasa. Bao hilo la pekee lilifungwa na mshambuliaji Michael Olunga katika dakika ya 65 na kumhakikishia mkufunzi Stanley Okumbi ushindi wake wa kwanza ugenini.