Makocha wa Wakenya wapata fursa ya kupata mafunzo kutoka kwa makocha wa timu ya Arsenal
23rd May, 2016
Makocha wa Kenya watapata fursa ya kupata kuongeza ujizi kwenye fani yao baada ya kampuni ya bahati na sibu ya Sportpesa kuzindua kliniki ya kutoa mafunzo ya soka ikishirikiana na timu ya uingereza ya arsenal. Makocha hao watapata mafunzo kutoka kwa makocha wa Arsenal kwa mda wa wiki moja. Makocha zaidi ya sitini wanaratajiwa kushiriki mafunzo hayo. Waandalizi wa mafunzo hayo wamewaomba washika dau katika soka nchini kuhakikisha kwamba wanakuza soka mashinani ili kuhakikisha ndoto ya kenya kushiriki kombe la dunia mwaka wa 2022.