Safaricom yazindua huduma mpya ya M-shwari
27th November, 2012
Kampuni ya mawasiliano ya safaricom imepiga jeki huduma zake za kifedha kwa kuzindua huduma mpya ya kuhifadhi fedha pamoja na kuomba mikopo. Huduma hiyo mpya kwa jina M-shwari itawawezesha wateja wa kampuni hiyo kuweka fedha katika benki pamoja na kuomba mikopo kwa kutumia simu zao za mkononi. Huduma hiyo inayotolewa kwa ushirikiano wa kampuni ya Safaricom na benki ya Commercial Bank of Africa itawawezesha wateja kuomba hadi mkopo wa shilingi alfu mia moja. Hata hivyo mikopo hiyo inapaswa kulipwa kwa muda wa siku 30.