1st October, 2020
Wizara ya michezo na uongozi wa soka katika kaunti ya Kisumu hii leo wamezindua rasmi awamu ya kwanza ya ujenzi wa uwanja mpya wa michezo utakaogharimu shilingi milioni 350. Uwanja huo utapewa jina la Jomo Kenyatta na unatarajiwa kutumika katika mechi za kimaitaifa.