18th February, 2021
Jamii ya Wamaasai na ambayo inasifika kwa ufugaji wa mifugo kama vile ngombe na mbuzi sasa inaonekana kuchukua mkondo mpya baada ya kuanza kufunga nguruwe. Kwa mujibu wa David ole palakuo na ambaye ni mojawepo wa wafugaji wa nguruwe kutoka eneo la Kimana, amehoji kwamba nguruwe ana manufaa mengi kushinda ng'ombe na pia faida kubwa ikizingatiwa kwamba anazaa watoto wengi kinyume na ng'ombe ambaye huzaa ndama moja tu. Aidha, Palakuo amedokeza kwamba kilimo cha ng'ombe kimekuwa na changamoto chungu nzima haswa wakati wa kiangazi ambapo ng'ombe wengi huangamia na kuwaacha wakulima wakikadiria hasara kubwa.