24th August, 2018
Serikali imesema kuwa haitoruhusu raia wa kigeni kutafuta leseni za kufanyia kazi wakiwa tayari humu nchini. Waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiangi ametoa amri hiyo akiwahutubia wakuu wa maswala ya usala katika chuo cha serikali huko kabete. Aidha Matiang'i amesema kuwa wafanyibiashara kutoka nchi za kigeni wataruhusiwa kuingia humu nchini iwapo tu watakuwa na vibali na leseni .