7th February, 2022
Wagombea wa viti vya kisiasa katika kaunti ya Nakuru sasa wamejitokeza kulalamikia kile wanachosema ni kulimbikiziwa viongozi na vyama vya kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Wagombea hao ambao ni wanachama wa vyama mbali mbali vya kisiasa wanataka viongozi wa miungano mikuu ikiwemo Azimio la Umoja, Kenya Kwanza na One Kenya Alliance kutowaleta watu waliowateua wao, na badala yake kuruhusu uchaguzi ulio huru na haki.