19th October, 2021
Kinara wa ODM Raila Odinga ameahidi kuimarisha soko la miraa la humu nchini na lile la kimataifa iwapo atachaguliwa kuliongoza taifa mwaka ujao. Akizungumza katika ziara yake ya eneo la Meru Odinga amesema atatumia usuhuba wake na marais wa mataifa ya DRC na Tanzania kuimarisha soko la zao hilo. Viongozi wa eneo hilo wakiongozwa na gavana wa Meru kiraitu murungi kwa upande wao wamesisitiza kujitolea kwao kusukuma azma ya odinga kumrithi rais Uhuru Kenyatta.