19th October, 2021
Mwili mwanariadha marehemu Agnes Tirop unatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa maiti hii leo katika eneo la iten kaunti ya elgeyo marakwet kubaini kiini cha kifo chake. Familia ya mwendazake itakuwa katika eneo hilo kusubiri matokeo ya uchunguzi. Mwanahabari elvis kosgey amekuwa akifuatilia taarifa hii na tutaungana naye hapo baadaye kwa maelezo zaidi.