15th October, 2021
Mshukiwa wa mauaji ya anayeshikilia rekodi ya dunia ya mbio za kilomita 10 Agnes Tirop amekamatwa usiku wa kuamkia leo katika maeneo ya Changamwe kaunti ya Mombasa. Kulingana na ocpd wa changamwe David Mathiu uchunguzi tayari umeanza huku mshukiwa huyo Ibrahim Rotich akitarajiwa kufikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika.