30th January, 2019
Askari gongo zaidi ya mia sita wa kampuni ya KK security wanaofanya kazi kwenye ubalozi wa Marekani hapa jijini Nairobi, wamegoma kulalamikia kile wanachodai unyanyasaji kutoka kwa mwajiri wao.
Wanadai kutolipwa marupurupu yao kwa zaidi ya miaka saba, hata baada ya mahakama kuamuru kwamba wapewe marupurupu hayo ambayo ni malipo ya saa za ziada za kufanya kazi.