5th November, 2018
Kesi ya mauaji ya kiongozi wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Meru Evans Njoroge maarufu kama Kidero imetajwa hivi leo katika mahakama kuu mjini Meru. Mshukiwa wa mauaji hayo Leakey Maina amabye ni afisa wa polisi wa Utawala alifanyiwa uchunguzi wa kiakili. Evans Njoroge ambaye alikuwa na umri wa miaka 23 aliuawawa kwa kupigwa risasi mwezi Februari akiwa katika mwaka wake wa mwisho.