2nd October, 2018
Shughuli za uchukuzi zimetatizwa kwa muda wa saa nane kwenye barabara ya kajiado?namanga kufuatia maandamano ya wafanyabiashara wa makaa waliofunga barabara wakilaumu serikali ya kaunti ya kajiado na wizara ya mazingira kwa kupiga marufuku biashara ya makaa.Wafanyabiashara hao ambao wengi ni akina mama wajane wanasema kwamba walikuwa wakipata mapato kutoka kwa biashara ya makaa ila sasa wanateseka. Aidha waandamanaji hao wamewashtumu maafisa wa polisi kwa kuzuilia makaa zaidi ya magunia 200 wakisema kuwa wanao wamekosa kwenda shule baada ya biashara zao kulemazwa.wakati uo huo, wahudumu wa magari wameelezea kughadhabishwa na maandamano hayo anyosema yamewaletea hasara huku wakilaumu polisi kwa kutoingilia kati.