1st October, 2018
Aliyekuwa mbunge wa Naivasha na mwenyekiti wa mamlaka ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevywa John Mututho ametoa wito kwa wabunge kupinga mswada wa sheria ya kuhalalisha ukuzaji na matumizi ya bangi nchini ambao umewasilishwa bungeni na mbunge wa kibra ken Okoth. Mututho kadhalika ametowa wito kwa wakenya na viongozi wa kidini kutoruhusu mienendo ya baadhi ya viongozi ambayo huenda ikapotosha jamii.