23rd July, 2018
Huku mgogoro kuhusu kuwahamisha watu waliovamia ardhi ya msitu wa Mau ukizidi kutokota maswali yanazidi kuibuka kuhusu dhamira ya serikali kujenga shule za umma zipatazo kumi na tano katika maeneo yenye utata ndani ya msitu huo.
Na sasa zinahitajika kubomolewa. Kama anavyoripoti mwandishi wetu elphas lagat, masomo katika shule hizo sasa yamesitishwa huku wenyeji wakiipa serikali changamoto ya kuwafichua watu ambao wanatajwa kuwa mabwenyenye walionyakuwa ardhi katika msitu huo kisha kuiza kwa raia.