10th July, 2018
Viongozi wa Jamii ya Pokot wamekashifu vikali utekaji nyara na mauji ya viongozi katika eneo hili. Wakizungumza katika hafla ya kumkaribisha nyumbani mwakilishi wa wadi ya silale nelson lotela aliyetekwanyara wiki iliyopita viongozi hao wameapa kuendelea kuishinikiza serikali kuwahakikishia usalama wao. Walikuwa wakizungumza katika eneo la Tiaty Kaunti ya Baringo.