2nd April, 2018
Washirika wa kanisa la roho Israel mjini Kisumu hapo jana walifanya sherehe zao kwa mbwembwe na vifijo katika mtaa wa Nyalenda. Washirika hao, wengine wakiwa walitoka maeneo ya Kendu Bay katika kaunti ya Homa Bay wakiwavutia wapita njia kwa namna walivyosherehekea kufa na kufufuka kwa yesu Kristo. Kutoka barabara moja hadi jingine katika mtaa wa Nyalenda, kulikuwa na densi ya kila aina ujumbne wao ukiwa kwa wakenya kudumisha amani.