15th February, 2018
Hatimaye rais Jacob Zuma amejiuzulu. Kiongozi huyo wa Afrika Kusini alitangaza kujiuzulu kwake hapo jana usiku, na kuelezea masikitiko yake jinsi chama tawala cha ANC kilivyofikia uamuzi wa kumtimua kwa madai ya masuala yaliyozingira na kughusia uadilifu wake uongozini. Asingefanya hivyo, hivi leo bunge la taifa hilo lilikuwa linajiandaa kupitisha hoja ya kutokuwa na imani naye.