Kauli za mawakili waliowatetea naibu rais William Ruto na mwanahabari Joshua arap Sang
6th April, 2016
Mawakili waliowatetea naibu rais William Ruto na mwanahabari Joshua arap Sang wameitaja kesi nzima iliyowakumba katika mahakama ya ICC kuwa dhaifu kuanzia mwanzo na kupelekea tangazo la kutupiliwa mbali jana jioni. Wakili wa ruto Karim Khan amesema kwamba upande wa mashtaka ulikosa ushahidi wa kutosha na badala yake kutegemea madai tu.