17th December, 2019
Muimbaji Kennedi Ombima maarufu King Kaka amejiwasilisha katika makao makuu ya upelelezi DCI baada ya kuwaarifu wakenya kupitia kwa mitandao yake ya kijamii kwamba alitakiwa kufika humo. King Kaka aliambatana na wasanii wengine pamoja na watetezi wa haki za binadamu. Hata hivyo ofisi ya DCI imesema kuwa haikumuita King Kaka kujiwasilisha ofisini mwao na kuwaomba wakenya kutotumia jina la ofisi za upelelezikwa njia isiyofaa.