6th September, 2018
Wenyeji eneo la Bisili katika kaunti ya Kajiado wanatoa wito kwa shirika la wanyama pori KWS kuwathibiti fisi ambao wamekuwa kero katika eno hilo.
Kulingana na wenyeji hao fisi wamekuwa wakiwala mifugo takribani kila siku.
Kisa cha hivi punde ni cha Bi Everliyne Naipanoi ambaye anaendelea kupokea matibabu baada ya kung'atwa na fisi siku nne zilizopita alipokuwa akiwaokoa mifugo wake waliokuwa wanavamiwa na fisi.