1st June, 2018
Maelfu ya wakenya wamesheherekea siku kuu ya madaraka kwenye kaunti tofauti humu nchini. Viongozi wametoa mwito kwa wakenya kuungana na kujiepusha na ufisadi. Kenya inaadhimisha miaka 55 ya kujitawala. Na licha ya Naibu Rais wa Afrika Kusini David Mabuza kuhudhuria sherehe hizo huko Meru, marais wa nchi jirani za Tanzania na Uganda hawakutuma hata wawakilishi wao. Kunani?