.
13th October, 2021
Mwanariadha Agnes Tirop aliyeiwakilisha kenya katika mashindano ya olimpiki kwa kushiriki mbio za mita 5000 mjini tokyo japani mwaka huu amefariki. Tirop amepatikana akiwa ameuawa mjini iteni. Kwa mujibu wa polisi, Tirop mwenye umri wa miaka 25 aliuawa kwa kudungwa kisu shingoni na mtu anayedaiwa kuwa mpenzi wake. Mshukiwa alitoweka katika mazingira tata.