.
16th September, 2021
Aliyekuwa waziri wa Michezo Hassan Wario tayari amelipa faini ya shilingi milioni 3.6 aliyopigwana mahakama baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya mamlaka na ufujaji wa pesa za umma. Ikimpata na hatia mahakama ilikuwa imemkatia kifungo cha miaka sita jela au faini ya shilingi milioni tatu nukta sita. Hata hivyo, mshatikwa mwenzake Stephen Soi ambaye alikuwa kiongozi wa ujumbe wa timu ya Kenya katika mashindano ya olimpiki mjini Rio mwaka 2016 alipewa adhabu kali zaidi ya kifungo cha miaka kumi jela au kulipa faini ya shilingi milioni 115.