22nd June, 2021
Mhandisi wa halmashauri ya ujenzi wa barabara kuu nchini Kenha David Mtilwa ametoa hakikisho kwamba sehemu ya barabara ya Waiyaki iliyoporomoka katika eneo la Kangemi inafanyiwa ukarabati, na kwamba wananchi wanaotumia barabara hiyo wasiwe na hofu kwani hakuna hatari. Sehemu hiyo iliporomoka hapo jana na kuwaacha takriban watu 10 wakiuguza majeraha madogo madogo.