×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Idara ya magereza nchini yaanza mchakato wa kuziondoa ndoo za kwendea haja kwa wafungwa

21st April, 2021

Idara ya magereza nchini imeanza mchakato wa kuziondoa ndoo za kwendea haja kwa wafungwa kwa kuwa zinachangia ongezeko la visa vya kuharisha katika vituo 120 vya magereza nchini. Kwa miaka kadhaa sasa wafungwa wamekuwa wakitumia ndoo hizo kujisaidia kisha kuondolewa wakati wa asubuhi, hali inayoathiri pia mazingira lakini sasa idara ya magereza imeamua kutengeneza vifaa vya namna ya kutumia vyema kinyesi kikichanganywa na taka za mbao kisha kuzalisha makaa ya kupika. Mradi huo utaanza kama majaribio katika magereza matano ya kwanza katika sehemu za Naivasha na Nakuru. Katibu mwandamizi katika idara ya serikali winnie guchu ameyasema hayo na kuongeza kuwa visa vya ongezeko la maradhi ya kuharisha vimekua vikipanda katika magereza nchini. Katibu wake Zeinab Hussein alisema tayari fedha za kuanzisha mradi huo zimetengwa.

.
RELATED VIDEOS