x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Upelelezi wa Kemsa: Kamati ya bunge la Seneti yataka Daktari Jonah Manjari kupelelezwa

30, Mar 2021

Wanachama wa kamati ya afya katika bunge la seneti sasa wanaitaka idara ya upelelezi DCI pamoja na kiongozi wa mashtaka kuwapeleleza mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya usambazaji dawa nchini, Kemsa, Daktari Jonah Manjari, mwenyekiti wa bodi hiyo Kembi Gitura pamoja na wanachama wa Kemsa kufuatia kupotea kwa zaidi ya shilingi billion 7 katika mamlaka hiyo. Kulingana na ripoti yao, maafisa hao hawakufuata sheria za ununuzi katika serikali na ndiposa pesa hizo zilipotea. Wakati uo huo, wanachama wa kamati ya uwekezaji wamekashifu hatua ya rais ya kumteua Kembi Gitura kuwa mwenyekiti wa mamlaka ya mawasiliano nchini licha ya kuwa ametajwa sana katika kashfa hiyo ya Kemsa.

Feedback