.
1st March, 2021
Watu wanaoishi na ulemavu katika kaunti ya nyamira wamewapa changamoto wabunge kupitisha sheria itakayoipa wizara ya uchukuzi ruhusa ya kuwajengea njia zao maalum kote nchini. Wanasema iwapo hilo litafanyika basi serikali itakuwa imewashughulikia vyema watu wanaoishi na ulemavu. Wakizungumza huko Sironga kaunti ya Nyamira, watu wanaoishi na ulemavu baada ya kutembea kwa kilomita tano kuadhimisha siku ya kiti cha magurudumu, wamesema kwa muda sasa wamesahaulika na kwamba ni vyema serikali iamke na kushughulikia masaibu yao.