.
7th October, 2020
Tukigeukia maambukizi ya korona nchini ni kuwa visa 321 vipya vya maambukizi ya virusi vya korona vimeripotiwa kwa muda wa saa 24 zilizopita. Hii ni kutokana na sampuli 4,342 zilizofanyiwa vipimo. Hii inafikisha jumla ya maambukizi ya korona nchini kufikia 39,907. Habari njema hata hivyo ni kuwa wagonjwa 4,222 wameripotiwa kupona kwa kipindi hicho. Hata hivyo, wagonjwa wengine 5 wamefariki kutokana na korona. Ni taarifa iliyotolewa na wizara ya afya nchini.