x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Wazee wa Akamba wafanya Tambiko sehemu ya Mikululo, walaani mapigano ya mzozo wa ardhi

30, Sep 2020

Wazee wa jamii za Akamba wamelaani vikali mapigano na mzozo wa ardhi ya malisho yaliokua yakiendelea sehemu ya Mikululo huko Makindu kaunti ya Makueni baina ya jamii zinazoishi kwenye mpaka wa kaunti za Kajiado na Makueni. Wakizungumza baada ya kufanya tambiko,wazee wa kundi la Thome wa mukamba wakiongozwa na mwenyekiti wao maingi kalii wamesisitiza kusitishwa kwa mzozo huo na kuwepo kwamwafaka baina ya jamii hizo kuhusu sehemu za malisho. Ardhi ya mikululo ambayo inamilikiwa na wenyeji wa makueni imekuwa ikitumika kwa malisho ya mifugo na kuendeleza kilimo cha kawaida tangu iidhinishwe na mahakama na kukabidhiwa wenyeji hawa kutoka kwa usimamizi wa shirika la Wanyamapori nchini. Awali kamati ya usalama kaunti ya Makueni ikiongozwa na kamishna wa kaunti Mohammed Maalim, ilizuru sehemu hio na kuhakikisha suluhu ya kudumu.

RELATED VIDEOS


Feedback