x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Maambukizi ya Korona : Wagonjwa 3 zaidi wafariki, wagonjwa 165 wapona Korona

16, Sep 2020

Watu 3 wameripotiwa kufariki kutokana na Virusi vya Korona na kufikisha idadi ya waliofariki kutokana na virusi hivyo kuwa 637. Kulingana na wizara ya afya watu 92 wameambukizwa virusi hivi kwa saa ishirini na nne zilizopita. Aidha watu 165 wameripotiwa kupona kutokana na virusi hivi, 60 walikuwa chini ya uangalizi wa nyumbani huku 105 kutoka vituo tofauti vya afya. Fauka ya hayo Wizara ya Afya imekanusha kuwepo kwa visa vya Korona kwa wageni wanoingia humu nchini, wakidai kuwa mikakati thabiti imewekwa kwenye viwanja vya ndege kuhakisha wale wanoingia nchini hawana virusi hivyo.

Feedback