2nd April, 2019
Wazazi walio na watoto wanaoishi na ulemavu wametakiwa kutumia vizuri nafasi za shule maalum ili kuona kwamba watoto hao wanaendelea na masomo kama watoto wengine. Akizungumza katika eneo la kerugoya kwenye shule ya wasioweza kusikia, aliyekuwa seneta wa kaunti ya kitui na aliye mwanachama wa tume ya kitaifa ya kushughulikia maswala ya walemavu david musila amesema kuna wasiwasi kutokana na hatua ya baadhi ya wazazi kuwaficha watoto wao wanaoishi na ulemavu majumbani. Musila hata hivyo amesema kuwa watoto hao wana haki ya elimu kupitia shule maalum za serikali na zile za mashirika yasiyo ya serikali.