x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Rais awapongeza wanajeshi Somalia kwenye hotuba yake

31, Mar 2016

Kwenye hotuba yake mbele ya wabunge na maseneta, Rais Kenyatta amesifia harakati za majeshi ya kenya nchini Somalia huku akiwaomba wakenya wote kuunga mkono harakati hizo. Aidha kenyatta amekosoa mienendo ya wanasiasa wa upinzani akisema kwamba wafaa kuelewa kwamba jukumu lao si kubadilisha wajibu wa upinzani kuwa mchezo wa sarakasi bali kuhakikisha taifa linaongozwa kwa njia ya kufaa. Aidha kwenye hotuba rais ameelezea baadhi ya ufanisi wa serikali haswa kwenye masuala ya miundo misingi akikiri kwamba amejizatiti kwenye sekta hiyo kukamilisha mipango iliyoanzishwa na serikali ya Rais Mwai Kibaki. Amepigia debe ongezeko la barabara nchini, ujenzi wa reli ya SGR, usambazaji nguvu za umeme hadi mashinani.

Feedback